SOKO LILILOKOSA WATEJA KWA SABABU YA UCHAFU

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Katika eneo moja la mjini kulikuwa na soko lililokuwa maarufu kwa kuuza matunda, mboga na vyakula mbalimbali. Kila siku wafanyabiashara walipata wateja wengi kutoka maeneo tofauti.

Baada ya muda wafanyabiashara na baadhi ya wateja walianza kutupa taka ovyo. Maganda ya matunda, mifuko ya plastiki na mabaki ya vyakula vilijaa kwenye njia za kupita. Harufu mbaya ilianza kusambaa na nzi waliongezeka kwenye vibanda vya chakula.

Wateja walianza kupungua kwa sababu wengi hawakupenda kununua bidhaa katika mazingira machafu.


Siku moja kikundi cha vijana waliokuwa wakifanya shughuli za kujitolea katika eneo hilo kiliamua kuzungumza na wafanyabiashara kuhusu hali ya soko. Walipendekeza kuweka mapipa ya taka na kuanzisha siku maalumu ya kufanya usafi.

Mwanzoni baadhi ya wafanyabiashara hawakuunga mkono wazo hilo lakini walipoona wateja wakianza kurejea baada ya usafi walibadilisha mtazamo wao.

Soko lilianza kuwa safi na kuvutia zaidi. Wafanyabiashara waligundua kuwa mazingira bora yalikuwa sehemu muhimu ya biashara zao.





emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments