Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Katika familia moja kila mtu alikuwa na shughuli zake kwenye simu. Baba alitazama video, mama alifuatilia mitandao ya kijamii huku watoto wakicheza michezo ya simu. Hata wakati wa chakulankila mmoja alikuwa akishughulika na kifaa chake.
Siku moja umeme ulikatika kuanzia mchana hadi usiku. Simu zilianza kuishiwa chaji na intaneti haikupatikana kwa sababu kifaa cha kusambaza mtandao nacho kilikuwa kimezimika.
Mwanzoni watoto walikasirika kwa kukosa michezo yao. Walijaribu kutafuta shughuli nyingine lakini hawakujua waanzie wapi.
Baba alipendekeza kila mtu akae pamoja sebuleni. Walianza kusimulia matukio ya utotoni, kucheza michezo ya kubahatisha na kukumbushana mambo yaliyowahi kuwafurahisha.
Walishangaa kuona muda ulivyopita bila mtu kuangalia simu.
Umeme uliporudi watoto walikimbilia kuchukua simu zao lakini mmoja wao alipendekeza waendelee na mazungumzo yao kwa muda.
Kuanzia siku hiyo familia ilianza kuwa na muda maalumu wa kukaa pamoja bila kutumia simu.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment