MWANGAZA WA MTAA ULIOPOTEA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Kwa muda mrefu watoto wa mtaa mmoja walikuwa wakicheza nje ya nyumba zao hadi jioni. Barabara ilikuwa na taa zilizowasaidia wakazi kuona vizuri hata giza lilipoingia.

Siku moja taa zote za barabarani zilizimika. Mwanzoni wakazi walidhani ni hitilafu ya umeme ya muda mfupi, lakini siku zilivyozidi kwenda, hali haikubadilika.

Giza lilipoanza kutawala, watoto walikosa sehemu salama ya kucheza jioni. Wafanyabiashara waliofungua maduka hadi usiku pia walianza kupata changamoto ya kuhudumia wateja.


Jambo lililowashangaza wakazi ni kwamba baadhi ya taa zilikuwa zimeharibiwa huku nyingine nyaya zake zikionekana kuchezewa.

Mkutano wa mtaa ulipoitishwa vijana walipendekeza kuanzisha kikundi cha kutoa taarifa mapema kuhusu miundombinu inayoharibika. Viongozi nao waliahidi kufuatilia suala hilo kwa mamlaka husika.

Baada ya muda taa zilirekebishwa na mtaa ukapata mwangaza wake tena. Wakazi waligundua kuwa kulinda miundombinu ya umma ni jukumu linalohitaji ushirikiano.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872






0/Post a Comment/Comments