MUDA UKIPOTEA HAURUDI NYUMA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Katika nyumba moja kulikuwa na mtoto aliyependa kuahirisha kila jambo. Akiambiwa aoshe vyombo aliahirisha, akiombwa afanye kazi za shule alisema atafanya baadaye.

Siku moja baba yake alimwomba ajiandae mapema ili waende kwenye sherehe ya familia. Mtoto huyo aliendelea kucheza mchezo wa simu akiamini bado alikuwa na muda mwingi.

Alipoangalia saa alishtuka kuona muda wa kuondoka umewadia. Akaanza kuoga haraka, kutafuta nguo na kuandaa viatu. Kwa sababu ya haraka alisahau vitu kadhaa muhimu.


Familia iliondoka bila yeye kwa sababu hakuwa tayari kwa wakati.

Alibaki nyumbani akiwa amekasirika na kujuta. Jioni baba yake aliporudi, alimweleza kuwa kuchelewa kwake hakukuathiri yeye pekee, bali familia nzima.

Kuanzia siku hiyo mtoto huyo alianza kutumia ratiba kupanga shughuli zake. Alijifunza kufanya mambo kwa wakati badala ya kusubiri dakika za mwisho.


emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments