Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Alipokuwa akipanga madaftari yake mtoto mmoja alikuta bahasha iliyokuwa imetoka shuleni. Ndani yake kulikuwa na taarifa ya kikao cha wazazi kilichohusu maendeleo ya wanafunzi.
Mtoto huyo aliogopa kumpa baba yake barua hiyo kwa sababu alikuwa amepata matokeo yasiyoridhisha katika baadhi ya masomo. Aliamua kuificha ndani ya droo akiamini kuwa hakuna mtu angegundua.
Siku ya kikao ilipofika baba yake alishangaa kwa nini hakukuwa na taarifa yoyote kutoka shuleni. Alipomuuliza mtoto alikaa kimya kwa muda kabla ya kukiri kuwa alikuwa ameificha barua.
Baba yake hakupendezwa na kitendo hicho lakini alimweleza kuwa kuficha matatizo hakutatui changamotoAlimwomba amweleze masomo yanayompa changamoto ili waweze kutafuta namna ya kumsaidia.
Mtoto alijisikia huru baada ya kusema ukweli. Aligundua kuwa angeweza kuzungumza na familia yake bila kuogopa kila mara anapokosea.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment