MTOTO ALIYECHUKUA PESA BILA RUHUSA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Mama mmoja alikuwa na biashara ndogo ya kuuza vitafunwa nyumbani. Kila siku aliweka fedha za mauzo kwenye droo maalumu kabla ya kuzipeleka benki.

Siku moja mtoto wake aliona noti kwenye droo hiyo. Alikuwa akitamani kununua gari dogo la kuchezea aliloliona kwenye duka la jirani. Bila kumuuliza mama yake alichukua sehemu ya fedha na kwenda kununua gari hilo.

Aliporudi nyumbani mama yake aligundua kuwa pesa hazikuwa sawa na mauzo aliyokuwa amefanya. Alimuuliza mtoto kama alijua kilichotokea lakini mtoto alikaa kimya.


Usiku huo mtoto alishindwa kufurahia kabisa gari lake jipya. Alijua kuwa pesa alizotumia hazikuwa zake. Hatimaye alimweleza mama yake ukweli na kuomba msamaha.

Mama yake alimweleza kuwa kuchukua pesa bila ruhusa ni kosa hata kama alikuwa na sababu ya kutaka kitu hicho. Walikubaliana kuwa angeanza kuweka akiba kidogo kidogo ili siku nyingine anunue vitu anavyovitaka kwa njia sahihi.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872





0/Post a Comment/Comments