Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Mtoto Aliaanza Kujichukia Kwa Sababu ya Muonekano Wake
Kila mtoto anapokuwa mbele ya kioo huona kitu tofauti kuhusu mwonekano wake. Kwa mtoto mmoja kioo kilikuwa kimekuwa chanzo cha huzuni badala ya kumsaidia kujitazama kwa furaha.
Alikuwa na mwili mkubwa kuliko watoto wengi wa umri wake. Wenzake walikuwa wakimpa majina ya kejeli na kumcheka kila walipokuwa wakicheza pamoja.
Mwanzoni alijaribu kupuuza maneno hayo lakini kadiri yalivyojirudia alianza kujitenga. Aliacha kushiriki michezo aliyokuwa akiipenda na akaanza kuvaa nguo pana ili kuficha mwili wake.
Siku mojabmama yake alimkuta akijitazama kwenye kioo huku akilia. Alipomuuliza tatizo mtoto alimweleza kuwa hakupenda muonekano wake kwa sababu ya maneno ya wenzake.
Mama yake alimfariji na kumweleza kuwa kila mwili una upekee wake na hakuna mtu anayepaswa kudhalilishwa kwa muonekano wake.
Pia alianza kumsaidia mtoto kujenga ujasiri na kumfundisha umuhimu wa kujithamini. Baadaye mtoto alianza tena kushiriki katika michezo na shughuli alizokuwa akizipenda.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment