MTEJA ALIYERUDISHA PESA ZILIZOZIDI

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Mtoto mmoja alienda dukani kununua madaftari na kalamu kwa ajili ya masomo yake. Alipofika nyumbani alikagua chenji aliyopewa na kugundua kuwa muuzaji alikuwa amemzidishia pesa.

Mwanzoni alifurahi kwa sababu angeweza kutumia pesa hizo kununua pipi. Lakini baada ya kufikiria alikumbuka kuwa huenda muuzaji angepata hasara kutokana na kosa hilo.

Alimweleza mama yake kilichotokea. Mama yake alimshauri arudi dukani na kurudisha pesa zilizozidi.


Mtoto alifanya hivyo muuzaji alishangaa sana kwa sababu hakutarajia mtoto angerudi baada ya kugundua kosa hilo.

Alimshukuru na kumwambia kuwa uaminifu wake ulikuwa wa thamani kubwa kuliko pesa alizorudisha.

Tukio hilo lilimfundisha mtoto kuwa kufanya jambo sahihi ni muhimu hata pale ambapo hakuna mtu anayekuangalia.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments