MGENI ALIYEFUNDISHA SOMO KUBWA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Jioni moja mvua kubwa ilinyesha mjini na kusababisha watu wengi kukimbilia kujisitiri kwenye vibanda vya biashara.

Mtoto mmoja aliyekuwa akitoka dukani alikutana na mzee aliyekuwa amesimama pembeni ya barabara akiwa amebeba mifuko mizito. Watu walikuwa wakipita bila kumjali kwa sababu kila mmoja alikuwa na haraka ya kujisitiri.

Mtoto huyo alisimama na kumuuliza kama angeweza kumsaidia kubeba baadhi ya mizigo yake. Mzee alikubali kwa furaha.


Walitembea pamoja hadi kwenye jengo lililokuwa karibu. Walipofika mzee alimshukuru na kumuuliza kwa nini aliamua kumsaidia wakati wengine walikuwa wakipita tu.

Mtoto akajibu kuwa aliona mtu mwenye uhitaji na akaamua kufanya kile alichoweza.

Mzee alitabasamu na kumwambia kuwa wema hauhitaji kuwa na pesa nyingi au nguvu kubwa. Wakati mwingine tendo dogo linaweza kumpunguzia mtu mwingine mzigo mkubwa.

Mtoto aliondoka akiwa na furaha kitambua kuwa kusaidia wengine ni jambo muhimu katika maisha.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872





0/Post a Comment/Comments