Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Shuleni kulikuwa na mashindano ya kuchora
picha. Kila mwanafunzi alitakiwa kuchora picha inayoonesha maisha ya familia
yake.
Mtoto mmoja alichora nyumba nzuri yenye
watu waliokaa pamoja wakicheka na kufurahi. Lakini mwalimu alishangaa kuona
kuwa kwenye picha hiyo hakukuwa na mtu aliyeshika simu.
Alipoulizwa kwa nini mtoto alieleza kuwa
nyumbani kwao kila mtu alikuwa akitumia simu yake wakati wa mapumziko. Hata
walipokuwa pamoja sebuleni hawakuwa wakizungumza.
Mwalimu alimsifu kwa kueleza ujumbe kupitia
mchoro wake. Baadaye aliomba ruhusa ya kuonesha picha hiyo kwenye mkutano wa
wazazi.
Wazazi wengi waliguswa na ujumbe huo.
Baadhi yao walianza kutenga muda maalumu wa kuzungumza na watoto wao bila
kutumia simu.
Mtoto huyo alifurahi kuona kuwa mchoro wake
ulikuwa umeibua mawazo mapya katika familia nyingi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment