Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Soko moja maarufu mjini lilikuwa na shughuli nyingi kila siku. Wafanyabiashara waliuza bidhaa mbalimbali huku wateja wakifika kutoka maeneo tofauti kufanya manunuzi.
Siku moja asubuhi wafanyabiashara walipofika sokoni walikuta maji yamejaa kwenye njia zote za kupita. Harufu mbaya ilitoka kwenye mifereji iliyokuwa imezibwa na taka na baadhi ya vibanda vilikuwa vimezungukwa na maji machafu.
Wateja walishindwa kufika kwenye baadhi ya maduka huku wafanyabiashara wakihofia bidhaa zao kuharibika.
Baada ya uchunguzi iligundulika kuwa mifereji ilikuwa imejaa mifuko ya plastiki, mabaki ya vyakula na uchafu mwingine uliokuwa ukitupwa ovyo.
Jambo hilo lilisababisha viongozi wa soko kuitisha mkutano wa dharura. Wafanyabiashara walikubaliana kuchangia gharama za kusafisha mifereji na kuweka utaratibu wa usafi wa kila siku.
Walishirikiana pia kuweka mapipa ya taka katika maeneo muhimu na kuzuia utupaji holela.
Baada ya siku kadhaa soko lilirejea katika hali yake ya kawaida. Wafanyabiashara walielewa kuwa usafi haukuwa suala la mwonekano pekee bali pia ulihusiana na usalama wa biashara zao.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment