Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kila mtoto katika mtaa wao alionekana kuwa na furaha kila kulipokuwa na sherehe za siku za kuzaliwa. Watoto walikuwa wakipeana mialiko kupanga mavazi na kujadili zawadi watakazonunua kwa marafiki zao.
Hata hivyo kulikuwa na mtoto mmoja ambaye mara nyingi aliachwa nje ya mipango hiyo. Hakuwahi kualikwa kwenye sherehe nyingi zilizofanyika mtaani jambo lililomfanya aanze kujitenga na wenzake.
Siku moja watoto kadhaa walikusanyika kwenye nyumba moja kusherehekea siku ya kuzaliwa ya rafiki yao. Mtoto huyo aliwaona wakiingia wakiwa na zawadi na nguo nzuri. Alisimama kwa mbali akitazama furaha yao huku akijiuliza kwa nini hakuwahi kukumbukwa.
Aliporudi nyumbani alikaa chumbani na kukataa hata chakula. Mama yake alipomuuliza alimweleza kuwa alihisi hakuna mtu aliyependa kuwa rafiki yake.
Mama yake alimfariji na kumwambia kuwa kutopata mwaliko hakumaanishi kuwa huna thamani. Pia alimshauri aanze kujenga urafiki kwa kuwa mwema, mkweli na mwenye kujali wengine.
Siku zilizofuata mtoto alianza kushiriki katika michezo ya pamoja na kuzungumza na watoto wengine. Taratibu alianza kupata marafiki waliomkubali.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment