“KUTENGANA KWA WAZAZI KUSIPUNGUZE UPENDO KWA WATOTO"


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Baada ya wazazi wake kutengana mtoto mmoja aliendelea kuishi na mama yake. Baba yake alikuwa akiishi sehemu nyingine na mara kwa mara alimtafuta ili waonane mwishoni mwa wiki.

Hata hivyo kila baba yake alipompigia simu na kumwomba waonane mtoto huyo alikuwa akitoa sababu mbalimbali za kutokwenda. Wakati mwingine alisema anaumwa mara nyingine alikuwa na kazi za shule.

Mama yake alianza kushangaa kwa nini mtoto alikuwa amebadilika ghafla. Siku moja aliamua kuzungumza naye kwa utulivu.

Mtoto alieleza kuwa kila alipokwenda kwa baba yake alikuwa akikutana na familia mpya na kujisikia kama hana nafasi tena katika maisha yake. Alihofia kuwa baba yake alikuwa amepata watoto wengine na kumsahau.


Mama yake alimsikiliza na kumweleza kuwa kutengana kwa wazazi hakumaanishi kuwa mtoto umepoteza nafasi yako katika maisha yake.

Baadaye baba yake alipotembelea nyumbani alikaa na mtoto huyo na kumhakikishia kuwa bado anampenda na anataka kushiriki katika maisha yake.

Mtoto alianza kuelewa kuwa anaweza kupendwa na wazazi wote wawili hata kama hawaishi pamoja.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments