Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Katika mtaa mmoja wa mjini kulikuwa na mti
mkubwa uliokuwa katikati ya kituo cha daladala. Kila siku abiria,
wafanyabiashara na watoto waliutumia mti huo kujikinga na jua kali wakati
wakisubiri usafiri.
Siku moja mfanyabiashara mmoja alinunua
eneo hilo kwa ajili ya kujenga fremu za maduka. Aliona mti huo ulikuwa kikwazo
cha upanuzi wa biashara yake hivyo akaamua kutafuta mtu wa kuukata.
Habari za kukatwa kwa mti ziliposambaa wakazi
wa eneo hilo walisikitika sana kwa sababu ulikua unawasaidia. Walisema mti huo
ulikuwa msaada mkubwa kwa watu waliokuwa wakisubiri magari hasa wazee na
wanawake waliokuwa na watoto wadogo.
Badala ya kuendelea kubishana baadhi ya
wakazi walipendekeza mfanyabiashara abadili mpangilio wa majengo ili mti ubaki.
Baada ya majadiliano mfanyabiashara huyo
alikaata na mti ulikatwa. Wakazi wa mtaa huo walitambua kuwa maendeleo mtu hayapaswi
kuingiliwa.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment