ALIKUA AKIKOPA VITU BILA KURUDISHA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Katika nyumba za kupanga watoto wengi walikuwa wamezoea kukopeshana vitu vidogo kama kalamu, vitabu, midoli na vifaa vya michezo.

Miongoni mwao alikuwa mtoto mmoja aliyekuwa na tabia ya kuomba vitu vya wenzake lakini mara nyingi hakuvirejesha. Wakati mwingine alidai amevipoteza na wakati mwingine alisahau kabisa alikoviacha.

Mwanzoni watoto walimvumilia kwa sababu walikuwa marafiki. Lakini kadiri siku zilivyopita walianza kukataa kumpa vitu vyao.

Siku moja alihitaji kalamu ya kuandikia zoezi lake la nyumbani. Aliwaomba marafiki zake kadhaa lakini wote walikataa kumkopesha.

Alirudi nyumbani akiwa amekasirika na kumweleza dada yake kuwa wenzake wamekuwa wabinafsi.


Dada yake alimuuliza kama alikuwa akirudisha vitu alivyokuwa akikopa. Swali hilo lilimfanya atafakari na kutambua kuwa yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa akiharibu uaminifu wa marafiki zake.

Siku iliyofuata alianza kuwarudishia wenzake baadhi ya vitu alivyokuwa amekopa na kuomba msamaha kwa vile vilivyopotea.

Polepole marafiki zake walianza kumwamini tena.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments