Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Matokeo ya mtihani yalipotolewa shuleni mwanafunzi mmoja alipata alama za chini kuliko alivyotarajia. Alipokea karatasi yake na kuiweka ndani ya begi bila kumwonesha mtu yeyote.
Alijua kuwa wazazi wake walikuwa wakimhimiza asome kwa bidii ili afanye vizuri. Aliogopa kuwaambia matokeo yake kwa sababu alidhani wangemkasirikia na kumlinganisha na wanafunzi wengine.
Kwa muda wa wiki mbili aliendelea kuishi kama kawaida. Kila alipoulizwa kuhusu matokeo alijibu kuwa bado hayajatangazwa.
Siku moja mama yake alipokuwa akipanga vitabu vyake aliikuta karatasi ya matokeo ikiwa imekunjwa ndani ya daftari.
Badala ya kumkaripia alimwita na kumuuliza kwa nini alikuwa ameamua kuficha matokeo hayo.
Mtoto alishindwa kujizuia na kuanza kulia. Alieleza kuwa alikuwa amejitahidi kusoma lakini hakuelewa baadhi ya masomo.
Mama yake alimfariji na kumweleza kuwa matokeo mabaya hayamaanishi kuwa umeshindwa maisha. Walikubaliana kutafuta msaada wa ziada katika masomo aliyokuwa na changamoto nayo.
Katika mtihani uliofuata alianza kufanya vizuri zaidi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment