Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Asubuhi moja mtoto mmoja aliamka na kugundua kuwa saa yake ya ukutani ilikuwa imesimama. Alifikiri bado ilikuwa mapema hivyo akaendelea kulala.
Alipoamka tena jua lilikuwa tayari limeingia dirishani.
Alioga haraka akavaa sare na kutoka bila hata kupata kifungua kinywa vizuri. Alipofika shuleni wanafunzi walikuwa tayari wameanza kipindi.
Siku hiyo aligundua jambo moja alikuwa ameanza kutegemea saa kuliko kujifunza kujitambua mwenyewe.
Jioni aliporudi nyumbani aliweka betri mpya kwenye saa. Lakini kabla hajalala aliweka pia alarm kwenye simu yake na kuandaa sare pamoja na vitabu vya kesho.
Asubuhi iliyofuata sliamka mapema.
Hakukimbia. Alipata muda wa kuoga, kula na kujiandaa vizuri.
Aligundua kuwa saa iliyosimama haikuwa tatizo kubwa. Tatizo lilikuwa kuacha kila kitu mpaka dakika za mwisho.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment