Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Asha na Mariam walikuwa marafiki wa karibu tangu walipoanza shule ya msingi. Walishirikiana vitabu, chakula na hata kusaidiana kufanya kazi za darasani.
Siku moja Asha alipokea ujumbe kwenye simu ya dada yake uliokuwa ukimsema Mariam. Bila kufikiria sana alipiga picha ya ujumbe huo na kuutuma kwenye kundi lao la wanafunzi.
Ndani ya muda mfupi wanafunzi wengi walikuwa wameusoma ujumbe huo na kuanza kumzungumzia Mariam. Alipogundua kilichotokea alihuzunika sana na kuamua kutomsemesha Asha.
Asha alipojaribu kuomba msamaha Mariam alimwambia kuwa kilichomuumiza zaidi si ujumbe wenyewe bali ni kuona rafiki yake akiusambaza bila hata kumuuliza ukweli wake.
Baada ya siku kadhaa Asha aligundua kuwa ujumbe ule ulikuwa umeeleweka vibaya na haukuwa na maana aliyodhani. Alijuta kwa kuharakisha kuusambaza.
Aliomba msamaha tena na kukubali kosa lake. Mariam alimpa nafasi ya kurekebisha urafiki wao lakini alimweleza kuwa uaminifu ungehitaji muda kujengwa upya.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment