Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Wakati wa mapumziko shuleni wanafunzi walikuwa wakisimulia kuhusu vitu walivyonunuliwa na wazazi wao. Mmoja alijivunia simu mpya mwingine viatu vya bei ghali na wengine nguo walizovaa mwishoni mwa wiki.
Mwanafunzi mmoja alikaa kimya. Alikuwa amevaa viatu vilivyochakaa na sare yake ilikuwa imeanza kufifia. Alipojaribu kujiunga na mazungumzo baadhi ya wanafunzi walimcheka na kumwambia kuwa hakuwa na vitu vya kujivunia.
Aliumia moyoni lakini hakujibu. Alirudi darasani na kuendelea na masomo yake kama kawaida.
Wiki chache baadaye shule ilifanya mashindano ya kitaaluma. Mwanafunzi ambaye alichekwa alikuwa akisoma kwa bidii kila siku alishika nafasi ya kwanza. Wanafunzi wengi walishangaa hasa wale waliokuwa wakimdhihaki.
Mwalimu aliwakumbusha kuwa thamani ya mtoto haipimwi kwa mavazi au vitu anavyomiliki bali hupimwa pia kwa tabia, juhudi na uwezo wake wa kujifunza.
Baada ya tukio hilo, baadhi ya wanafunzi waliomba msamaha kwa naye aliendelea kujituma bila kuwadharau wengine.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment