Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Ilikuwa Jumatano jioni. Baada ya kurudi kutoka shule mtoto mmoja aliingia nyumbani akiwa amechoka. Alibadilisha sare, akaweka begi pembeni na kuanza kufanya kazi zake za shule.
ABaadaye alitoka kwenda dukani kununua mkate. Aliporudi aligundua kuwa mlango wa nyumba ulikuwa haujafungwa vizuri.
Alishtuka. Alikumbuka kwamba kabla ya kutoka alikuwa ameufunga haraka bila kuangalia kama umefungika kabisa.
Aliingia ndani na kukagua vitu vyake. Q na kitu kilichopotea lakini moyo wake ulikuwa ukipiga kwa nguvu
Alipofika nyumbani mama yake alimweleza kilichotokea.
Badala ya kumfokea mama yake alimfundisha jambo muhimu kila mtu anaweza kufanya kosa lakini muhimu ni kujifunza kutokana nalo.
Kuanzia siku hiyo mtoto huyo alianza kuwa makini zaidi. Kabla ya kuondoka nyumbani alihakikisha milango na madirisha vimefungwa vizuri. Pia alianza kukumbuka kuzima vifaa vya umeme ambavyo havikutumika.
Wiki chache baadaye mdogo wake alisahau kufunga mlango wa nyuma.
Mtoto huyo hakumcheka wala kumfokea. Alimweleza kwa utulivu kwa nini ni muhimu kuwa makini.
Alikuwa amejifunza kutokana na kosa lake.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment