Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Mtoto mmoja alipanda daladala kwenda shule akiwa na mzazi wake. Kwa sababu ya msongamano wa abiria mara nyingi alikaa kwenye kiti cha nyuma na kuweka begi lake mapajani.
Siku moja daladala lilipokuwa limejaa mzee mmoja alipanda akiwa amechoka. Hakukuwa na kiti kilichobaki.
Mtoto huyo alimtazama kwa muda. Alikuwa amechoka pia lakini alikumbuka maneno ambayo mama yake alikuwa akimwambia mara nyingi. “Heshimu watu na fikiria hali ya mwingine".
Aliinuka na kumpa mzee nafasi yake.
Mzee huyo aliketi na kumshukuru safari ikaendelea.
Kesho yake mtoto huyo alifanya jambo lilelile kwa mwanamke aliyekuwa amembeba mtoto mdogo. Baada ya siku kadhaa akaanza kugundua kwamba watu wengine pia walikuwa wakianza kuwapa nafasi wale waliokuwa wanahitaji zaidi.
Hakukuwa na zawadi wala mtu aliyemlipa kwa kufanya hivyo. Lakini kila alipomsaidia mtu alijisikia vizuri.
Hatimaye alielewa kwamba heshima na utu vinaonekana zaidi katika matendo madogo ya kila siku.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment