MTOTO ALIYEOGOPA KUULIZA MASWALI


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Darasani wanafunzi walikuwa wakijifunza somo la hisabati ambalo wengi wao waliliona kuwa gumu. Miongoni mwao alikuwepo mtoto aliyekuwa akipata shida kuelewa baadhi ya maswali lakini aliogopa kuinua mkono na kumuuliza mwalimu kwa sababu alihofia kuchekwa na wenzake.

Kila mwalimu alipouliza kama kuna mwanafunzi ambaye hajaelewa mtoto huyo alikaa kimya hata alipokuwa hajafahamu somo. Aliporudi nyumbani alijaribu kufanya kazi alizopewa lakini mara nyingi alishindwa kuzimaliza.

Kadiri siku zilivyopita alama zake zilianza kushuka. Mama yake alipogundua mabadiliko hayo alizungumza naye na kugundua kuwa mtoto wake alikuwa na hofu ya kuuliza maswali darasani.


Siku iliyofuata mama yake alimshauri kuwa kuuliza swali si ishara ya kutokujua bali ni njia ya kujifunza. Alimwambia kuwa hata watu wazima huuliza maswali wanapohitaji kuelewa jambo fulani.

Mtoto alianza kupata ujasiri kidogo kidogo. Siku moja mwalimu alipokuwa akifundisha alinyanyua mkono na kuuliza kuhusu swali ambalo hakulielewa. Mwalimu alimjibu kwa utulivu na kutoa mfano mwingine ili wanafunzi wote waelewe.


Kwa mshangao wake wanafunzi wengine walimshukuru kwa kuuliza swali hilo kwa sababu nao walikuwa hawajaelewa.

Kuanzia siku hiyo mtoto alianza kushiriki zaidi darasani. Alipoona jambo gumu aliomba msaada badala ya kukaa kimya. Baada ya muda uaelewa wake uliongezeka na matokeo yake yakaanza kuboreka.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments