MTOTO ALIYEMCHEKA MWENZAKE BILA KUJUA ANACHOPITIA


Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Asubuhi moja wanafunzi walikuwa wamekusanyika uwanjani wakijiandaa kuingia madarasani. Miongoni mwao alikuwepo Baraka mtoto aliyependa kucheka na kufanya utani na wenzake. Siku hiyo mwanafunzi aliingia shuleni akiwa amevaa sare iliyochakaa na viatu vilivyokuwa vimeanza kuchanika.

Baraka alipomwona alianza kumcheka mbele ya wanafunzi wengine.

“Kwa nini umevaa viatu vya namna hiyo Huna viatu vingine nyumbani" Baraka aliuliza huku akicheka.

Baadhi ya wanafunzi walijiunga naye lakini Juma hakujibu. Alishusha kichwa na kuingia darasani kimya kimya.

Siku zilizofuata aliendelea kumtania kila alipokutana naye. Hakujua kuwa Juma aliishi na bibi yake baada ya kumpoteza mama yake, huku baba yake akiwa mbali akitafuta kazi. Bibi yake alijitahidi kumpeleka shule licha ya changamoto za maisha.

Siku moja mwalimu aliwaagiza wanafunzi kufanya kazi ya kikundi. Baraka na mwanafunzi mgeni walipangiwa kufanya kazi pamoja. Mwanzoni Baraka hakufurahia uamuzi huo lakini aliamua kushirikiana naye.

Walipokuwa wakifanya kazi Baraka aligundua kuwa mwenzake alikuwa mwerevu sana na alielewa masomo kwa haraka. Juma alimsaidia kuelewa maswali kadhaa ambayo yalikuwa yakimpa shida.



Baada ya masomo Baraka alimuuliza kwa nini hakuwahi kujibu nilipo kuwa na kucheka. Mwanafunzi yule alimweleza kwa utulivu kuwa hakuwa na uwezo wa kununua viatu vipya kwa wakati huo lakini alikuwa akijitahidi kusoma ili kutimiza ndoto zake.

Maneno hayo yalimfanya Baraka ajisikie aibu. Alitambua kuwa alikuwa akimhukumu mwenzake bila kujua hali aliyokuwa akiipitia.

Siku iliyofuata Baraka alimwomba msamaha mbele yao wawili na kuacha tabia ya kumcheka. Taratibu wakawa marafiki na Baraka akajifunza kumheshimu kila mtu bila kujali mavazi au hali ya familia yake.

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

0/Post a Comment/Comments