Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Watoto wanapokutana pamoja.mara nyingi hutafuta michezo itakayowafanya wafurahie muda wao wa mapumziko. Hata hivyo si kila mchezo unahitaji mpira, vifaa vya kuchezea au eneo kubwa. Wakati mwingine maneno machache yanaweza kuanzisha mchezo wenye furaha na kuwasaidia watoto kujifunza mambo mapya.
Siku moja wakati wa mapumziko watoto watatu walikuwa wamekaa chini ya mti baadala ya kwenda kucheza mpira. Walikuwa wamechoka na masomo na hawakujua cha kufanya. Mmoja wao akapendekeza waanze mchezo wa kukamilisha maneno.
Sheria ilikuwa rahisi. Mtoto mmoja angesema neno lililoachwa wazi kisha wengine wangejaribu kulikamilisha kwa kutafuta herufi au silabi inayokosekana.
Mchezo ulianza kwa neno MA__I. Kila mmoja alianza kufikiri. Baada ya muda mfupi mmoja wao akasema “MAJI!”
Wenzake walifurahi kwa sababu jibu lilikuwa sahihi. Wakafuata na neno KI__BU ambalo lilipaswa kuwa KITABU.
Kadiri mchezo ulivyoendelea watoto walianza kutumia maneno mapya waliyokuwa wamejifunza darasani. Walipokutana na neno gumu walijaribu kusaidiana badala ya kukata tamaa.
Baada ya muda waligundua kuwa walikuwa wamejifunza maneno mengi bila hata kuhisi kama walikuwa darasani.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment