Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Mchana mmoja watoto kadhaa walikuwa wamekaa pamoja nyumbani baada ya kumaliza kufanya kazi zao za shule. Kwa kuwa hawakuwa na mchezo wa kucheza mmoja wao alipendekeza waanze kuulizana mafumbo ili kuona nani angeweza kupata majibu sahihi kwa haraka.
Mchezo ulianza kwa swali rahisi: Nina meno mengi lakini sili chakula. Mimi ni nani?
Watoto walianza kutaja vitu mbalimbali lakini mmoja wao alijibu kwa kujiamini kuwa ni sega. Wote walicheka na kuendelea na fumbo lililofuata.
Kadiri mchezo ulivyoendelea maswali yalizidi kuwa magumu. Kila mtoto alijitahidi kufikiri kabla ya kutoa jibu. Wakati mwingine walikosea lakini hawakukata tamaa. Walijifunza kutokana na majibu ya wenzao na kuendelea kujaribu.
Baada ya muda watoto waligundua kuwa mchezo huo haukuwa wa kushindana pekee bali pia uliwasaidia kutumia akili zao, kujifunza vitu vipya na kushirikiana.
Tangu siku hiyo waliamua kuwa kila wanapopata muda wa mapumziko wangecheza mafumbo badala ya kukaa bila kufanya chochote.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment