Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Katika jiji la Mwanza aliishi mtoto wa miaka kumi na mmoja aliyekuwa na tabia ya kulaumu wengine kila alipofanya kosa. Akivunja kitu nyumbani alimlaumu mdogo wake. Akipoteza vifaa vya shule aliwashutumu wenzake. Tabia hiyo iliwafanya watu wengi kushindwa kumwamini.
Siku moja mama yake alimkabidhi simu yake na kumwomba aitunze vizuri alipokuwa akijiandaa kwenda kazini. Mtoto aliichukua simu na kwenda kukaa sebuleni. Alipokuwa akiitumia iliteleza mikononi mwake na kuanguka sakafuni. Kioo chake kilipasuka.
Mtoto aliingiwa na hofu akaiweka simu mezani na kuendelea na shughuli nyingine kana kwamba hakuna kilichotokea.
Mama yake alipogundua simu imeharibika aliuliza kilichotokea. Badala ya kusema ukweli mtoto alimlaumu mdogo wake aliyekuwa chumbani wakati wa tukio hilo.
Mdogo wake alijitetea kwa machozi lakini kaka yake aliendelea kukataa kuhusika. Mama yao hakuwakaripia. Aliwaambia kuwa kusema ukweli ni muhimu kuliko kujaribu kujificha nyuma ya makosa ya wengine.
Mama yake alimpongeza kwa kukubali kosa lake kisha akamweleza kuwa kila mtu anaweza kukosea lakini ni muhimu kuwajibika kwa matendo yake.
Mtoto alimwomba mdogo wake msamaha na kuahidi kubadilika. Kuanzia siku hiyo alianza kujifunza kukubali makosa yake bila kulaumu wengine. Taratibu familia yake ilianza kumwamini tena.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment