KUJIAMINI KULIKOGEUKA KIKWAZO CHA MAFANIKIO


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Kila mama alipomwomba mtoto wake afanye kazi ndogo nyumbani alikataa kusaidiwa na kusema angeweza kufanya kila kitu mwenyewe. Alitaka kufua nguo zake, kuandaa sare za shule na hata kupika bila kupewa maelekezo.

Mwanzoni mama yake alifurahia kuona mtoto akijiamini. Hata hivyo kadiri siku zilivyopita alianza kugundua kuwa mtoto huyo hakupenda kushauriwa. Alipoonywa kuhusu kosa fulani alikasirika na kudai kuwa watu hawakumwamini.

Siku moja aliamua kuandaa chakula akiwa peke yake. Kwa kutokufuata maelekezo aliyokuwa amepewa aliweka chumvi nyingi na kuharibu chakula.


Alipomwita mama yake amsaidie alitarajia kukosolewa. Badala yake mama alimfundisha jinsi ya kupima viungo na kumweleza kuwa kujitegemea hakumaanishi kukataa msaada.

Mtoto alianza kuelewa kuwa kujiamini ni jambo zuri lakini kusikiliza ushauri wa wengine humsaidia mtu kujifunza na kufanya mambo vizuri zaidi.

Kuanzia siku hiyo alijitahidi kufanya mambo mwenyewe huku akiwa tayari kupokea msaada na maelekezo.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments