Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kila siku Shukuru alitumia dakika chache kuchora picha nyuma ya madaftari yake. Alipokuwa darasani wakati mwingine alisahau kuandika maelezo ya mwalimu kwa sababu alikuwa akiboresha michoro yake.
Siku moja mwalimu wa sanaa alikusanya madaftari ya wanafunzi ili kukagua kazi zao. Alipofungua daftari la Shukuru alishangazwa na michoro mizuri aliyokuta ndani yake.
Badala ya kumkaripia mwalimu alimshauri Shukuru atenge muda maalumu wa kuchora na muda wa kusoma masomo mengine. Pia alimpa nafasi ya kushiriki mashindano ya sanaa yaliyokuwa yakiandaliwa shuleni.
Shukuru alianza kufanya mazoezi baada ya kumaliza kazi za shule. Alipofika siku ya mashindano alichora picha iliyovutia majaji na kushinda nafasi ya pili.
Alifurahi sana lakini jambo lililomfurahisha zaidi ni kuona kuwa angeweza kuendeleza kipaji chake bila kuacha masomo yake.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment