KIPAJI KINAHITAJI MUDA, MAZOEZI NA KUJIAMINI


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Daftari moja lilikuwa limejaa michoro pembeni mwa kurasa. Badala ya kuandika tu majibu ya maswali, mtoto huyo alikuwa akichora magari, nyumba, watu na vitu alivyoviona njiani.

Alijua anapenda kuchora lakini hakutaka mtu yeyote azione picha zake.

Shuleni alipokuwa amemaliza kazi mapema aliendelea kuchora kimya kimya. Siku moja mwalimu alipita karibu na dawati lake na kuliona daftari hilo.

Mtoto huyo alishtuka na kulifunga haraka. Alifikiri mwalimu angemkemea kwa kuchora wakati wa kipindi. Lakini mwalimu alimuuliza kwa utulivu kwa nini alikuwa akichora sana.


Alieleza kuwa alikuwa akipenda kuchora akini alikuwa anaogopa wanafunzi wengine kumcheka.

Mwalimu alimwambia kuwa na kipaji hakumaanishi kila mtu atakipenda lakini hakupaswi kukificha kwa sababu ya hofu ya maoni ya wengine.

Kuanzia siku hiyo alianza kutenga muda maalumu wa kuchora baada ya kumaliza kazi zake za shule.

Miezi michache baadaye shule ilitangaza mashindano ya kuchora. Alitumia kile alichokuwa akifanya kwa siri kwa muda mrefu kutengeneza mchoro wake.


Hakushinda nafasi ya kwanza lakini mchoro wake uliwekwa kwenye ubao wa matangazo wa shule.

Kwa mara ya kwanza, hakuhisi aibu kuhusu kile alichokuwa akipenda.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments