KELELA ZILIZOFUKUZA NDEGE SHULENI


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Katika shule moja ya mjini kulikuwa na miti mingi iliyokuwa kivutio cha ndege mbalimbali. Kila asubuhi wanafunzi walifurahia kusikia sauti za ndege walipokuwa wakijiandaa kuingia madarasani.

Hata hivyo baadhi ya wanafunzi walianza tabia ya kupiga kelele, kurusha mawe kwenye miti na kuharibu viota vya ndege kwa ajili ya kujifurahisha.

Baada ya muda ndege walianza kupungua. Miti iliyokuwa ikisikika kwa sauti za ndege kila asubuhi ikawa kimya.

Siku moja mwalimu wa sayansi aliwauliza wanafunzi kama walikuwa wamegundua mabadiliko hayo. Wengi walikiri kuwa hawakuwa wamewahi kufikiria madhara ya matendo yao kwa viumbe wengine.


Mwalimu aliwaeleza kuwa ndege husaidia kusambaza mbegu za mimea na kudhibiti baadhi ya wadudu. Aliwasisitizia kuwa mazingira yanahitaji kulindwa ili viumbe wote waendelee kuishi kwa usalama.

Wanafunzi waliamua kuweka sheria za kulinda miti na viota vya ndege. Waliacha kurusha mawe na kuanza kuelimisha wenzao kuhusu umuhimu wa kutunza viumbe hai.

Polepole shule ikawa sehemu tulivu na salama zaidi kwa ndege na wanafunzi.




emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments