Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Usiku ulikuwa umeingia na kila mtu nyumbani alikuwa ameenda kulala. Lakini taa ya sebuleni ilikuwa bado imewashwa.
Mtoto mmoja alitoka chumbani kwenda kunywa maji. Alipoiona taa ile aliendelea na safari yake bila kuizima.
Asubuhi mama yake alipokuwa akifanya usafi aligundua kuwa taa ilikuwa imewaka usiku mzima. Alimuuliza kama alijua aliyeiacha.
Mtoto huyo alikumbuka kwamba ndiye aliyeiacha ikiwa imewaka. Aliona aibu kwa sababu alikuwa ameambiwa mara kadhaa kuzima taa na vifaa vya umeme ambavyo havitumiki.
Mama yake hakumkaripia. Alimweleza kwamba kutumia umeme bila sababu kunaongeza matumizi ya nyumbani na pia ni muhimu kuwa makini na vifaa vya umeme kwa usalama.
Kuanzia siku hiyo mtoto huyo alianza kufanya ukaguzi mdogo kabla ya kwenda kulala. Alizima taa zisizohitajika akahakikisha televisheni imezimwa na akawa makini na vifaa vingine vya umeme.
Baada ya muda tabia hiyo ikawa sehemu ya maisha yake ya kila siku.
Aligundua kuwa kuwajibika nyumbani hakuhitaji kusubiri mtu mzima akuambie kila kitu.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment