JIFUNZE KUPANGA VITU VYAKO NA KUACHA VISIVYO HITAJIKA

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Alipofika nyumbani kutoka shule mtoto huyo aliuweka mkoba wake chini na kukaa kimya.

Mama yake alipojaribu kuunyanyua alishangaa kuona ulikuwa mzito sana. Ndani kulikuwa na vitabu, madaftari, chupa ya maji, nguo za michezo na vitu vingine ambavyo mtoto huyo alikuwa amebeba kwa siku kadhaa bila kuvitoa.

Kesho yake mama yake alimsaidia kupanga mkoba wake.

Walitoa karatasi zilizokuwa hazihitajiki, madaftari yaliyomalizika na vitu ambavyo havikuwa vya shule. Mtoto huyo akaacha ndani ya mkoba vitu alivyohitaji kwa siku hiyo tu.

Alipofika shuleni alihisi tofauti. Alitembea kwa urahisi zaidi na hakulalamika tena kuhusu maumivu ya mabega.


Mwalimu alipowaambia wanafunzi watunze vitu vyao vizuri mtoto huyo alikumbuka jinsi alivyokuwa akibeba vitu visivyohitajika kila siku.

Kuanzia hapo alianza kupanga begi lake kila jioni kulingana na ratiba ya kesho.

Baada ya muda hakubeba tena vitu kwa mazoea.

Alijifunza kwamba wakati mwingine mzigo hauwi mzito kwa sababu ya vitu vingi tu bali kwa sababu tunashindwa kuchagua kile tunachohitaji.




emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments