Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kwa wiki kadhaa Kelvin alikuwa akichelewa
kurudi nyumbani baada ya shule. Mama yake alipomuuliza sababu alidai kuwa
alikuwa akisoma na marafiki zake. Ukweli ni kwamba alikuwa akitumia muda mwingi
kucheza michezo ya kompyuta kwenye duka lililokuwa karibu na shule.
Kadiri siku zilivyopita Kelvin alianza
kutumia fedha za chakula kucheza michezo na kupuuza kazi za shule. Siku moja mwalimu
alimwonya kwa kutowasilisha kazi alizopewa.
Jioni moja alipofika nyumbani alimkuta mama
yake akiwa amekaa sebuleni akimsubiri. Alikuwa amepigiwa simu na mwalimu kuhusu
maendeleo ya mwanawe. Kelvin alipojaribu kutoa sababu nyingine mama yake
alimwomba aseme ukweli.
Mama yake alimweleza kuwa kucheza si kosa lakini
kupuuza masomo na kusema uongo ndio kosa na linaleta matatizo. Kelvin alijutia tabia yake na
kuahidi kubadilika.
Katika siku zilizofuata Kelvin alianza
kukamilisha kazi zake na kurudi nyumbani kwa wakati. Aligundua kuwa angeweza
kufurahia michezo bila kuharibu masomo yake.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment