Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Siku moja mtoto alipokuwa akisafisha begi lake la shule alikuta karatasi iliyokunjwa ndani ya kitabu cha zamani. Alipoifungua alishangaa kuona ilikuwa barua iliyoandikwa na mama yake miaka kadhaa iliyopita kabla hajaanza shule.
Katika barua hiyo mama alikuwa ameandika ndoto zake kuhusu mtoto wake. Alitamani akue akiwa mwaminifu, mwenye bidii na anayejali watu wengine. Pia aliandika kuwa huenda familia yao isingekuwa na kila kitu lakini upendo na elimu vingekuwa urithi muhimu kwake.
Mtoto alisoma barua hiyo mara kadhaa. Kwa siku za hivi karibuni, alikuwa amekata tamaa ya kusoma kwa sababu aliona baadhi ya wenzake walikuwa na vifaa vizuri zaidi na walionekana kufanya vizuri kuliko yeye.
Jioni hiyo, alimwomba mama amsaidie kupanga ratiba ya masomo. Alianza kusoma kwa bidii na kuacha kujilinganisha na wengine.
Miezi michache baadaye, aliboresha matokeo yake. Alipomweleza mama kuhusu barua ile, mama alitabasamu na kumkumbatia.
Mtoto aligundua kuwa wakati mwingine maneno ya upendo yanaweza kumsaidia mtu kuona uwezo aliokuwa ameusahau.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment