ADELADIUS MAKWEGA
OFISI
YA RAIS – IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA
DODOMA
Dodoma, Ijumaa, Oktoba 30, 2026.
Picha hii imepigwa katika Uwanja wa Mashujaa, Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo ya ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali pamoja na barabara ya lami katika Mji wa Serikali Mtumba.
Hafla hiyo ya kihistoria ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wageni waalikwa, ikiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Jamhuri ya Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço.
Uzinduzi huo ulihusisha miundombinu muhimu ya Serikali, ikiwemo:
“Majengo ya ofisi za Wizara 26.Majengo ya Taasisi 11 za Serikali.Barabara za lami zenye urefu wa kilomita 57.1.”
Katika picha hii anaonekana Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Rais – Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Ndugu Firimin Msiangi (wa kwanza kutoka kulia), akiwa pamoja na viongozi wenzake wakati wa kuimbwa kwa Wimbo wa Taifa wa Angola.
Sehemu inayokumbuka na kipekee ya hafla hiyo ilikuwa wakati wa kuimbwa kwa Wimbo wa Taifa wa Angola, unaojulikana kwa jina la ‘Angola Avante’, wenye maana ya ‘Angola Iwe Mbele’ kwa lugha ya Kiswahili.
Wimbo huo unaimbwa kwa lugha ya Kireno (Portuguese) na ulianza kutumika rasmi mwaka 1975, kufuatia kupatikana kwa uhuru wa taifa hili.
Wimbo wa ‘Angola Avante’ unabeba ujumbe muhimu wa kizalendo na kihistoria unaosisitiza:
“Uhuru wa Taifa: Kutambua na kuthamini uhuru wa Angola. Umoja na mshikamano: Kuhimiza umoja, ushirikiano na mshikamano miongoni mwa wananchi.Uzalendo: Kujenga moyo wa kulitumikia na kulitetea taifa. Historia ya mapambano: Kukumbuka juhudi na mapambano ya wananchi wa Angola katika kudai uhuru wao.”
Kuimbwa kwa wimbo huo katika hafla hiyo kulikuwa sehemu ya itifaki ya kitaifa na kidiplomasia, ikionesha heshima kwa Taifa la Angola na kuimarisha uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya Tanzania na Angola.
makwadeladius@gmail.com- 0717649257
.gif)


.gif)
Post a Comment