Adeladius Makwega wa Mbagala
Kumbukumbu tunalinda, kwa sheria na taratibu,
Sera zote twazingatia, kwa kanuni na taratibu,
Katika umma twasimamia, nyaraka na kumbukumbu,
Kwa uadilifu twatenda, tukilinda kila hazina.
Waasisi tunawahifadhi, kwa heshima na uaminifu,
Nyerere na Karume pia, ni hazina ya uhai,
Vitu vyao tunakusanya, kwa upendo na uadilifu,
Fikra zao tunadumisha, kwa kizazi cha baadaye.
Mifumo tunaiweka, ya nyaraka na kumbukumbu,
Ili kazi ziende vyema, kwa ufanisi na tija,
Ushauri tunautoa, wa kuhifadhi kwa utaratibu,
Rekodi muhimu zilindwe, zisipotee katika njia.
Viwango tunaviweka, kwa nyaraka na kumbukumbu,
Miongozo tunaiandaa, ya kutunza kwa uangalifu,
Taasisi zote za umma, zifuate huo utaratibu,
Huduma ziwe bora zaidi, kwa manufaa ya taifa.
Nyaraka tunakusanya, historia isiangamie,
Urithi andishi wa taifa, milele udumu nao,
Kumbukumbu tunahifadhi, kwa vizazi vikaone,
Hazina hii ya taifa, kwa kesho tusiiache.
Majanga tunayakabili, kwa mipango ya maandalizi,
Urejeshaji twaandaa, kumbukumbu zisipotee,
Majalada tunayapima, yenye thamani yabaki,
Yasiyo na umuhimu, kwa sheria yatokomee.
Teknolojia twatumia, nyaraka kuzihifadhi,
Upatikanaji uwe rahisi, kwa wote wanaohitaji,
Nakala halisi zilindwe, zisiharibike na wakati,
Historia yetu idimu, kwa vizazi vyetu vyote.
Umma tunauhamasisha, huduma zetu uzijue,
Nyaraka na kumbukumbu, kwa manufaa uzitumie,
Kwa pamoja tulinde hazina, taifa letu lisimame,
Idara yetu yatumikia, historia isije ikome.
0717649257







Post a Comment