Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
"Trrr! Trrr! Trrr!" Kengele ya shule ililia na wanafunzi wakaanza kutoka madarasani kwa furaha.
Miongoni mwao alikuwa Kevin, mvulana wa darasa la sita aliyependa sana teknolojia. Kila aliporudi nyumbani alifanya kazi zake za shule kisha alitumia muda kujifunza kupitia kompyuta na intaneti.
Siku moja mwalimu wa Sayansi alitangaza mashindano ya kubuni kifaa kitakachosaidia kutatua tatizo katika jamii. Wanafunzi wengi walihofia kushiriki akini Kevin aliamua kujaribu.
Kwa wiki mbili alifanya utafiti akachora michoro na kutengeneza mfano wa kifaa cha kukusanya maji ya mvua kwa matumizi ya bustani za shule.
Siku ya mashindano ilipofika Kevin aliwasilisha wazo lake kwa kujiamini. Majaji walivutiwa na ubunifu wake. Ingawa hakushika nafasi ya kwanza alipata tuzo ya "Wazo Bora la Ubunifu"
Aliporudi nyumbani alimwambia baba yake "Leo nimejifunza kwamba kushinda si kila kitu. Kilicho muhimu ni kuthubutu kujaribu"
Baba yake alitabasamu na kusema "Kila mafanikio makubwa huanza na hatua moja ya ujasiri".
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872




Post a Comment