USIMDHARAU MTU KWA HALI YAKE YA MAISHA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Rehema alikuwa mwanafunzi wa darasa la nne. Kila siku alitembea zaidi ya kilomita mbili kwenda shuleni. Viatu vyake vilikuwa vimechakaa sana kiasi kwamba vidole vyake vilionekana.

Siku moja mvua kubwa ilinyesha akiwa njiani. Alifika shuleni akiwa amelowa na viatu vyake vikaharibika kabisa. Baadhi ya wanafunzi walimcheka lakini mwalimu aliwaambia "Tusimdhihaki mwenzetu kwa sababu ya hali yake"

Baada ya masomo wanafunzi walikubaliana kuchangia kiasi kidogo cha fedha walichokuwa nacho. Mwalimu naye akaongeza sehemu iliyobaki. Mwishoni mwa wiki walimnunulia Rehema jozi mpya ya viatu.


Alipovivaa Rehema alitabasamu kwa furaha. Aliwashukuru wenzake na kuahidi kusoma kwa bidii ili siku moja naye aweze kuwasaidia watoto wengine wenye uhitaji.

Miaka kadhaa baadaye Rehema alifanikiwa kuwa mwalimu. Kila mwaka aliwasaidia wanafunzi waliokuwa na changamoto za kupata sare, viatu na vifaa vya shule akisema "Wema niliooneshwa nikiwa mtoto ndio ulionipa nguvu ya kuendelea".


emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872





0/Post a Comment/Comments