USIMCHEKE MTOTO KWA SABABU AMEKOSEA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Darasani kulikuwa na mtoto mmoja aliyekuwa akipenda kucheka kila mwenzake alipokosea.

Mwanafunzi akijibu swali vibaya alicheka. Mwingine akianguka wakati wa michezo alicheka zaidi. Hakuwahi kufikiria kuwa siku moja angejikuta katika hali hiyo.

Siku moja mwalimu aliwaomba wanafunzi wasome mbele ya darasa. Aliposimama alipatwa na hofu. Alianza kusoma lakini akachanganya baadhi ya maneno.

Darasa lilicheka. Uso wake ukabadilika kwa mara ya kwanza alihisi maumivu aliyokuwa akiwaongezea wenzake kila walipokosea.


Alikaa chini akiwa kimya. Baada ya kipindi alitazama daftari lake na kufikiria sana aligundua kuwa kosa la mtu halikuwa sababu ya kumdhalilisha.

Kuanzia siku hiyo alibadilika. Mwanafunzi alipokosea alianza kumtia moyo badala ya kucheka. Alipomwona mwenzake akishindwa jambo alimsaidia.

Polepole wenzake wakaanza kumwamini tena.

Alijifunza kuwa maneno na matendo madogo yanaweza kumuumiza mtu au kumjenga.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments