Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kila asubuhi mtoto mmoja mwenye miaka kumi alikuwa akienda shule akiwa na hamu ya kujifunza. Alikuwa anapenda sana kusoma lakini kulikuwa na somo moja lililokuwa linampa changamoto.
Kila alipofanya zoezi la somo hilo alipata makosa mengi. Wenzake walipoanza kuelewa yeye bado alihitaji muda zaidi. Hali hiyo ilimfanya aanze kujiona hawezi.
Siku moja alirudi nyumbani akiwa ameshika daftari lake na kulia kimya. Alilitazama daftari hilo na kufikiria kuacha kabisa kujifunza.
Baadaye aliamua kujaribu tena. Alianza kusoma kidogo kidogo kila siku. Aliposhindwa kuelewa aliomba msaada kutoka kwa mwalimu na wenzake.
Wiki zilipopita alianza kuona mabadiliko. Makosa yalipungua na majibu yake yakaanza kuwa sahihi.
Siku moja mwalimu alipotoa zoezi alifanikiwa kulimaliza vizuri. Alifurahi sana kwa sababu alikumbuka siku ambazo alikuwa akilia kwa sababu ya somo hilo.
Kuanzia hapo alijifunza kuwa mafanikio hayaji kwa siku moja. Wakati mwingine mtu huhitaji kujaribu tena kujifunza na kuendelea mbele hata anapokutana na changamoto.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment