Adeladius Makwega- Ofisi ya Rais Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa DODOMA
Katika Mkutano wa 14 wa TRAMPA ambacho ni Chama cha Menejimenti cha Watunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka nchini Tanzania umenogeshwa na kuwavutia wengi baada ya kufanyika mchezo wa Kuigiza wenye igizo fupi na kugani wimbo uliofanya na mwanamuziki Mrisho Mpoto, huku katika igizo hili lilishangiliwa mno na wadau wote ukumbini mapema Septemba 23, 2026.
Katika mchezo huu uliokuwa na maudhui ya umuhimu wa kada za Watunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka za taasisi mbalimbali huku mhusika wake mkuu akiwa dada mtunzaji wa kumbukumbu alionesha umahiri wa kazi hii.
Mwanamuziki Mrisho Mpoto ambaye alionekana katika hatua za mwisho wa mchezo huu , alisisitiza kuwa ili taifa kufikia dira yake ya 2050 lazima watunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka wanapaswa kupewa kipao mbele wasiachwe nyuma.
Mrisho Mpoto alisisititiza,
“Hawa siyo watunzaji wa makaratasi bali watunzaji wa kumbukumbu zeye tija kwa taifa iwe leo, kesho na hata siku zijazo. Naiomba serikali na wadau wote tuithamini kada hiii mara moja.”
Mkutano huu wa mwaka wa 2026 wa TRAMPA unafanyika jijini Dodoma kukiwa na wadau zaidi 1000.
makwadeladius@gmail.com) 0717649257












Post a Comment