UMUHIMU WA KUMFUNDISHA MTOTO NIDHAMU TANGU AKIWA MDOGO


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Malezi bora huanza tangu mtoto akiwa mdogo. Miongoni mwa mambo muhimu ambayo wazazi na walezi wanapaswa kumfundisha mtoto ni nidhamu. Nidhamu humsaidia mtoto kuelewa tofauti kati ya jambo sahihi na lisilo sahihi, kuheshimu wengine na kuwajibika kwa matendo yake.

Mtoto anayefundishwa nidhamu tangu utotoni hukua akiwa na tabia nzuri. Hujifunza kusalimia, kuheshimu wakubwa, kushirikiana na wenzake na kufuata maelekezo. Tabia hizi humsaidia nyumbani, shuleni na katika jamii kwa ujumla.

Aidha nidhamu humjengea mtoto uwezo wa kujidhibiti. Kwa mfano mtoto hujifunza kusubiri zamu yake, kutatua migogoro kwa utulivu na kudhibiti hasira au hisia nyingine. Uwezo huu ni muhimu katika kujenga mahusiano mazuri na kufaulu katika masomo na maisha ya baadaye.


Wataalamu wa malezi wanashauri wazazi kutumia njia za upendo, mawasiliano na mfano mzuri wanapomfundisha mtoto nidhamu. Badala ya kutumia adhabu kali ni vyema kumweleza mtoto sababu ya sheria zilizowekwa na matokeo ya kuvunja sheria hizo. Mtoto anapofanya jambo jema anapaswa kupongezwa ili kuhimiza tabia nzuri.

Pia ni muhimu wazazi kuwa na msimamo unaofanana katika malezi. Mtoto huelewa kwa urahisi anapopata maelekezo yanayofanana kutoka kwa walezi wake. Hali hii humjengea mazingira salama ya kujifunza na kukua.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments