SUNGURA NA KASA WENYE URAFIKI


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Aliishi sungura mwepesi sana na kasa mwenye subira. Kila siku walicheza pamoja msituni. Siku moja waliona ndege mdogo ameanguka kutoka kwenye kiota chake.

Sungura alikimbia haraka kutafuta majani laini huku kasa akitembea polepole kwenda kumwita mama ndege. Walifanya kazi kwa ushirikiano. Mwishowe mama ndege alifika na kumrudisha mtoto wake salama kwenye kiota.

Mama ndege aliwashukuru sana na kusema "Urafiki ni moyo wa kusaidiana na kuvumilivu na sio kukimbia haraka”

Kuanzia siku hiyo sungura alijifunza kuwa kasi si kila kitu na kasa alifurahi kuona kwamba kila mmoja ana kipawa chake.


emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872








0/Post a Comment/Comments