SIKU AMBAYO HAKUCHUKUA SIMU


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Jioni moja umeme ulikatika ghafla katika nyumba moja ya mjini. Mtoto aliyekuwa amezoea kutumia muda wake mwingi kwenye simu alibaki amekaa kitandani akiiangalia simu yake iliyokuwa imebaki na betri kidogo.

Hakukuwa na intaneti, hakukuwa na kitu cha kumtazama.

Kwa mara ya kwanza alitoka chumbani na kukaa sebuleni. Alianza kusaidia kupanga vitabu vilivyokuwa vimetapakaa mezani. Baadaye alichukua daftari lake na kuanza kuchora.

Kadiri muda ulivyopita aligundua kuwa hakuhitaji simu kila wakati ili kujisikia vizuri.



Usiku huo umeme uliporudi simu yake ilianza kutoa arifa nyingi. Aliichukua akaitazama kwa muda mfupi, kisha akaiweka pembeni.

Alirudi kwenye daftari lake na kuendelea kuchora.

Kuanzia siku hiyo alianza kujipangia muda wa kutumia simu. Alitenga muda wa kusoma kuzungumza na familia, kufanya kazi za nyumbani na kupumzika bila simu.

Baada ya muda aligundua kuwa siku zake zilikuwa zimejaa mambo mengi zaidi kuliko alivyokuwa akifikiri.


emakulalatemsafiri@gmail.com

0653903872



0/Post a Comment/Comments