SIKU AMBAYO ALIKOSA MTU WA KUMWAMBIA

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Kila asubuhi mtoto mmoja aliingia darasani akiwa mchangamfu. Alizungumza na wenzake alicheka na kushiriki kwenye masomo. Kwa nje kila kitu kilionekana kuwa sawa.

Lakini kulikuwa na jambo moja ambalo hakuna aliyelijua.

Kila alipokuwa na jambo lililomsumbua aliliweka moyoni.

Siku moja alifanya kosa kubwa shuleni. Aliogopa sana kwamba angeadhibiwa hivyo akaamua kukaa kimya. Aliporudi nyumbani hakutaka hata kula.

Usiku huo alikaa kwenye meza yake na kufungua daftari. Badala ya kufanya kazi za shule aliandika kila kitu kilichokuwa moyoni mwake.


Alipoimaliz alihisi nafuu kidogo Kesho yake mwalimu aligundua kuwa hakuwa kama kawaida. Hakumlazimisha kueleza kila kitu. Alimpa tu nafasi ya kuzungumza pale alipokuwa tayari.

Hatimaye mtoto huyo alieleza kilichokuwa kimemsumbua.

Mwalimu alimsikiliza bila kumkatiza Kwa mara ya kwanza mtoto huyo aligundua kuwa si kila tatizo linapaswa kubebwa peke yako.

Baada ya siku hiyo alianza kujifunza kuzungumza na watu aliowaamini pale alipokuwa na jambo linalomsumbua.Na polepole tabasamu lake lilirudi.




.emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments