MTOTO TO ALIYEJIFUNZA KUOMBA MSAADA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Kila siku baada ya shule mtoto mmoja alipenda kukaa na kufanya kazi zake za shule peke yake. Alikuwa na tabia ya kuamini kwamba kila jambo alipaswa kulimaliza mwenyewe.

Aliposhindwa kuelewa somo fulani hakumuuliza mwalimu. Alipokuwa amesahau kitabu,hakumuomba mwenzake. Hata alipokuwa na jambo lililomsumbua moyoni alikaa kimya.

Mwanzoni aliona kujitegemea kwake kuwa jambo zuri. Lakini kadiri siku zilivyopita alianza kupata ugumu katika masomo yake. Kazi zilianza kumzidi na alifanya makosa mengi kwa sababu aliogopa kuomba msaada.


Siku moja mwalimu aliona mabadiliko hayo na kumweleza kuwa kuomba msaada si ishara ya udhaifu. Mtu anaweza kuwa jasiri na bado akahitaji msaada kutoka kwa wengine.

Maneno hayo yalimfanya afikirie. Siku iliyofuata alipokutana na swali gumu darasani alinyanyua mkono na kumuuliza mwalimu. Kwa mara ya kwanza hakuhisi aibu.

Baada ya muda alianza kuwa huru zaidi kuuliza pale ambapo hakuelewa. Masomo yake yakaanza kuimarika na hata wenzake wakaanza kumuona kama mtoto anayejua kutambua wakati wa kujisaidia.


Aligundua jambo muhimu hakuna mtu anayejua kila kitu na hakuna ubaya kusema naomba unisaidie.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments