MTOTO ANAYELALA SANA MCHANA NI KAWAIDA AU KUNA TATIZO?


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Usingizi ni sehemu muhimu ya maisha ya mtoto. Mtoto anapolala mwili na ubongo hupata nafasi ya kupumzika na kuendelea kukua. Hata hivyo mzazi anaweza kujiuliza anapomwona mtoto akilala muda mrefu wakati wa mchana.

Kwa watoto wadogo kulala mchana ni jambo la kawaida. Mahitaji ya usingizi hutofautiana kulingana na umri. Watoto wachanga hulala muda mwingi zaidi wakati watoto wanapokua muda wa usingizi wa mchana hupungua hatua kwa hatua.

Usingizi wa kutosha humsaidia mtoto kuwa makini, kujifunza, kukumbuka na kuwa na hisia zilizo sawa. Mtoto anayekosa usingizi anaweza kuwa mchovu, mwenye hasira au kushindwa kuzingatia vizuri.


Hata hivyo mzazi anapaswa kuangalia hali ya mtoto kwa ujumla. Ikiwa mtoto alianza ghafla kulala kupita kiasi, hana hamu ya kula, anaonekana dhaifu au ana dalili nyingine za ugonjwa hali hiyo haipaswi kupuuzwa.

Wazazi wanaweza kumsaidia mtoto kupata usingizi mzuri kwa kuweka ratiba inayofanana kila siku. Mazingira ya kulala yanapaswa kuwa tulivu, salama na yenye mwanga mdogo wakati wa kulala. Pia ni vizuri kuepuka michezo yenye msisimko mkubwa kabla ya muda wa kulala.

Kulala mchana si tatizo kwa mtoto bali ni sehemu ya ukuaji wake. Kinachohitajika ni kuhakikisha anapata usingizi wa kutosha kulingana na umri wake na kuangalia mabadiliko yoyote yasiyo ya kawaida.


emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872




0/Post a Comment/Comments