Mkutano wa 14 wa TRAMPA Umechangamka

 

Adeladius Makwega






Ofisi ya Rais – Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, DODOMA.

 

Hali ya uchangamfu imetawala katika Mkutano wa 14 wa TRAMPA unaofanyika jijini Dodoma, ambapo, Septemba 23, 2026, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kufungua rasmi mkutano huo ulioanza Septemba 21, 2026.

 

Mapema, Septemba 23, 2026, hali ya uchangamfu imetawala katika mkutano huo, ambapo Mwanakwetu ameshuhudia vibwagizo kadhaa vilivyoibua hamasa miongoni mwa washiriki.

 

Huu ni mkutano wa 14 wa TRAMPA, ukitanguliwa na mikutano 13 ya awali. Mkutano huu unafanyika jijini Dodoma kuanzia Septemba 21 hadi 25, 2026.

 

TRAMPA ni Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania, kilichoanzishwa rasmi mwaka 2013 kwa lengo la kuwaunganisha pamoja wataalamu wa kada hii.

Kwa sasa, jukwaa hili linaongozwa na Bi. Devota Mrope, ambaye ndiye Mwenyekiti.


makwadeladius@gmail.com
0717649257

 

 

 

0/Post a Comment/Comments