Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Siku moja baada ya masomo watoto wengi walitoka darasani kwa haraka. Mmoja wao alisahau mkoba wake chini ya dawati.
Kesho yake alipofika shuleni aligundua kuwa hakuwa na mkoba. Alitafuta kila mahali lakini hakuuona.
Alianza kuingiwa na hofu kwa sababu ndani kulikuwa na vitabu, madaftari na kalamu zake zote.
Alipofika darasani aliona mkoba wake ukiwa juu ya meza ya mwalimu. Mwalimu alimwambia kuwa mtoto mmoja alikuwa ameupata baada ya shule na kuuleta ofisini bila kuchukua kitu chochote.
Mtoto huyo alifurahi sana. Baada ya masomo alimuona yule mtoto aliyekuwa ameleta mkoba. Hakujua amshukuru kwa maneno gani. Alimshukuru tu kwa moyo wote.
Jambo hilo lilimfanya afikirie: kama mtu angechukua vitu vyake, angejisikiaje?
Kuanzia siku hiyo alianza kuwa mwangalifu zaidi na vitu vyake. Lakini pia alijifunza kutunza mali za wengine kama ambavyo angependa mali zake zitunzwe.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment