Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kila alipokuwa akienda shule mtoto mmoja alikuwa na tabia ambayo watu wengi waliipenda. Hakupenda kuona mwenzake akiwa hana kitu ambacho yeye angeweza kumsaidia.
Siku moja wakati wa mapumziko alikaa pembeni akila maandazi mawili aliyokuwa amepewa na mama yake. Alipomwona mwenzake akiwa amekaa kimya bila chakula hakusubiri kuulizwa. Aligawanya maandazi yake na kumpa moja.
Siku nyingine mwanafunzi mwenzake alisahau kalamu. Badala ya kumcheka alimpa kalamu yake ya ziada. Alipofika nyumbani na kumweleza mama yake, mama yake alimwambia.
“Ukarimu haupimwi kwa ukubwa wa kitu unachotoa bali kwa moyo unaotumia kutoa"
Maneno hayo yalimfanya aelewe kuwa mtoaji si mtu mwenye vitu vingi pekee. Hata mtoto mwenye kitu kidogo anaweza kumsaidia mwingine.
Tangu siku hiyo aliendelea kushirikisha wenzake vitabu, chakula, vifaa vya shule na hata muda wake. Polepole watoto walianza kujifunza kutoka kwake.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment